Shirika la Umeme Tanzania - Tanesco, limesema Makali ya kukatika kwa Umeme jijini Dar es Salaam pamoja na mikoa inayounganishwa na gridi ya Taifa itaanza kupungua, baada ya jana kuwasha mtambo mwingine wa symbion na kuingiza megawati 35.
Mkurugenzi wa shirika la Umeme nchini Felchemi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm amesema, hali ya kukatika kwa umeme itaendelea kupungua kabla ya jumapili baada ya kuingiza na kuwasha mtambo wa umeme wa kinyerezi, ambao utaingiza katika gridi ya taifa megawati 70 pamoja na megawati 20 za mtambo mwingine wa symbion.
Aidha Bw,Mramba amesema hali ya uzalishaji wa umeme unaotokana na vyanzo vya maji uko katika hali mbaya, kutokana na kupungua kwa kina cha maji kwa Asilimia 81.3 na kuzalisha chini ya kiwango.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu huku wataalamu wa shirika hilo wakiendelea kusimamia uingizaji wa gesi katika mitambo na kuahidi kazi hiyo itakamilika tarehe 20 mwezi huu na hali ya umeme itaimarika zaidi.