Baraza la Usimamizi wa Mazigira nchini NEMC limekifunga kiwanda cha China papers Co-operation Limited cha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa muda usiojulikana kutokana na kutokidhi vigezo vilivyowekwa na Serikali ikiwemo suala la usafi wa mazingira.
Miongoni mwa sababu zilizochangia kufungwa kiwanda hicho ambacho kinatengeneza Karatasi maalumu (Toilet Paper) ni pamoja na kuwepo kwa mazingira machafu hali ambayo inahatarisha afya za wafanyakazi na wakazi wanaoishi maeneo ya kuzunguka kiwanda hicho.
Wakiwa katika kiwanda hicho majira ya shubuhi Wafanyakazi wa Nemc walishangazwa na mazingira hatarishi ya wafanyakazi kiwandani hapao na kuamua kukifunga kiwanda hicho.
Pamoja na kufungwa kwa kiwanda hicho hadi hapo watakaporekebisha kasoro zilizoonekana lakini pia wanapaswa kulipa faini kiasi cha shilingi mioni 80 kama faini ya makosa yaliyobainika kiwandani hapo.
Kufuatia hali hiyo uongozi wa kiwanda hicho umelalamikia faini liyotolewa na NEMC ingawa umeahidi kutekeleza kwa haraka baadhi ya maagizo.
Hatimaye ziara ya kushtukiza ya wafanyakazi wa NEMC ikafika katika kiwanda cha ngozi cha Moshi Tanarise kilichopo mjini hapo ambacho kimekuwa kikitiririsha maji ovyo ambayo yanadiwa kuwa na kemikali na hivyo kuhatarisha viumbe hai.
Kwa miaka nenda rudi kiwanda hicho cha ngozi kimekuwa kikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kutoka na harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka kiwandani hapo na kuwakera wananchi.
Ujio wa Nemc Mkoani kilimanjaro pengine huenda ukasaidia kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi wanaozunguka viwanda hivyo ambavyo vimekuwa vikitiririsha maji yenye kemikali na kuwatia hofu wananchi wanaoishi maeneo hayo.
