Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi taifa Mizengo Pinda amewataka watanzania kutofanya makosa kuwachagua wagombea wasiokuwa na uwezo wakuongoza na kuleta maendeleo ya kweli akidai kuwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dokta John Magufuli ndiye kiongozi mwenye uwezo wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa awamu ya tano.
Pinda amezungumza hayo katika vijiji vya Mwamapuli na Usevya kwenye mikutano ya hadhara ya kumnadi mgombea urais wa CCM pamoja na mbunge wa jimbo la Kavuu Dokta Kikwembe.
Akihutubia mikutano hiyo ya hadhara Waziri Mkuu Pinda Ambae pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi taifa anasema wapo baadhi ya wagombea ambao wamekuwa wakibeza maendeleo yaliopo uku akiwataka wananchi kumchagua dakta Pombe Magufuli kuendeleza yale yote yaliaoachwa na serikali ya awamu ya nne.
Nae Mgombea wa Ubunge jimbo la Kavuu Purudenciana Kikwembe anawakumbusha wapiga kura hao kutosahau ahadi alizowapa na kuahidi kuzitimiza.
Mkuu wa mkoa wa katavi Dakta Ibrahimu Msengi na mwenyekiti wa chama mkoa Abdalah Msele wanazungumzia suala la udini.