Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu wa sekondari hatua inayoathiri kukua kwa kiwango cha taaluma kutokana na walimu hao kuishi mbali na shule wanazofundisha.
Kutokana na hali hiyo wilaya imeanza kutafuta misaada kutoka kwa wafadhili kwa kuwa kiwango kinacholetwa na serikali kila mwaka kwa ajali ya ujenzi wa nyumba hizo ni kidogo kikilinganishwa na mahitaji yaliyopo.
Mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondary Mkinga hapo wilayani Mkinga Mkoani Tanga yaliambatana na harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba za waliumu.
Uhaba wa nyumba za walimu katika wilaya hii unaonekana ni chanmgamoto inayoathiri maendeleo ya elimu.
Ofisa elimu wa sekondari Omari Kombo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Mboni Mgaza anawataka wazazi kuona namna ya kushiriki katika kutatua tatizo hilo.
Wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari shuleni hapo wamesema waalimu wao wanakaa katika vijiji vya jirani ,na kuongeza kuwa jambo hilo limewaathiri kitaaluma.
Kwa sasa wilaya hiyo ina nyumba 32 za walimu wa shule za sekondari.