Mgombea udiwani kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Egnatio Mtawa amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa diwani wao, atahakikisha anatetea haki za wanyonge na kulitaja kudi la vijana wanaoendesha bodaboda katika kata hiyo kuwa miongoni mwa atakao watetea
Amesema hayo jana wakati akizindua kampeni zake katika viwanja vya setendi ya zamani Tandala na kuongeza kuwa pamoja na kutetea kundi hilo tangu akiwa madarakani kama diwani kwa kipindi cha miaka mitano (2010-2015) amekuwa akitetea haki za madereva bodaboda kutokana na kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani na kusema pamoja na mambo mengine atakayoyafanya hilo litakuwa ni miongoni bila kujali itikadi zao za vyama
Mgombea huyo amesema endapo atapata madaraka pia atahakikisha mji wa Tandala unajengwa kwa mpangilio mzuri kwa kuwa ni mji unao kuwa huku akihakikisha kodi mbalimbali zinazotozwa na serikali kwa wananchi hasa wafanyabiashara ambazo zinaonekana kuwa ni kero wanapambana nazo
"Unajua hili suala limekuwa pia likizungumzwa na mgombea urais wetu Dkt John Pombe Magufuli na mimi niwe wazi kabisa nitamuunga mkono kwa kuhakikisha wafanyabiashara wa hasa mama ntilie na wengine hawanyanyasiki na kodi ndogondogo ambazo ni kero kwao na wakati mwingine zinaanzishwa na watendaji wa serikali ambao sio waaminifu na wanaojiamulia mambo yao wenyewe" amesema Mtawa
katika uzinduzi huo alisindikizwa na wagombea wengine wa chama cha mapinduzi katika kata mbalimbali akiwemo Daniel Okoka anayegombea kata ya Lupila ambapo amesema kwa mwaka 2010 wilaya ya Makete iliongezewa kata mpya tano Ikiwemo ya Tandala, na mpaka sasa Kata ya Tandala iliyokuwa ikiongozwa na Mtawa ndiyo pekee iliyofanikisha kujenga ofisi za kata huku nyingine zikisuasua
"Mimi sioni haja ya ninyi kumnyima kura Mtawa, kama ofisi ya kata mnayo, barabara ya kwenda Lupalilo sekondari ilikuwa mbovu sasa hivi inapitika, hapa mna stendi, na mengine mengi ambayo bila usimamizi wake mngekuta hamna, hapa mpeni kura yeye tu" amesema Okoka
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Makete Erica Sanga amesema kutokana na utendaji kazi wa Matawa bila shaka wananchi watamchagua tena kuongoza kwa kipindi kingine cha 2015-2020, huku akimuombea kura zote kutoka kwa wananchi wa ccm na wengine kutoka vyama vya upinzani akikitaja chama cha Chadema
Uzinduzi wa kampeni hizo kwa mgombea huyo wa CCM zimeanza rasmi na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 18 mwaka huu
Wananchi wakifuatilia kampeni za mgombea udiwani Tandala wakiwa wameketi juu ya gari
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Makete Erica Sanga akimuombea kura Egnatio Mtawa
Mgombea udiwani kata ya Tandala akiserebuka jukwaani muda mchache kabla ya kuanza kuhutubia
Mgombea udiwani kata ya Tandala Egnatio Mtawa (CCM) akimtambulisha jukwaani mpinzani wake wa kwenye kura za maoni na kusema hawana ugomvi wowote
Mgombea udiwani Tandala kupitia CCM akimtambulisha mkewe kwa wananchi waliofika kwenye kampeni zake