Mgombea ubunge katika Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro
kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Peter Lijuakali amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita
baada ya kukutwa na hatia ya kumtukana ofisa mtendaji wa
kata.
Mahakama wilayani Kilombero imetoa hukumu hiyo baada ya
kuridhika na ushahidi ambao umethibitisha kuwa mgombea
huyo alimtukana ofisa mtendaji wa kata ya Ifakara, Afuley
Mwenga.
Hata hivyo, Oktoba 12, mwaka huu, mahakama hiyo itaamua juu ya tuhuma nyingine
inayomkabili Lijuakali ya kutishia kumuua mtendaji huyo wa Ifakara.
Wafuasi wa Chadema waliokusanyika mahakamani hapo walionyesha nyuso za furaha kwani
walidhani mahakama hiyo ya wilaya ingemhukumu mgombea wao kwenda jela.