Rose Mhando amesema hana furaha katika maisha ya Ukristo

Rose Mhando amesema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka. Pia Rose aliwaponda baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

"Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu. Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose. 

Source: GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo