Mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo
katika Jimbo la Manyovu mkoani
Kigoma, Goodluck Kimali amenusurika kifo
baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka
likiwa kwenye msafara wa Kiongozi wa chama
hicho, Zitto Kabwe.
Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Nyalulanga, Kata ya Busunzu wilayani
Kibondo katika Mkoa wa Kigoma, juzi, usiku.
Tukio hilo lilihusisha gari aina ya Nissan katika msafara uliokuwa na magari
manane ukitoka Kasulu kwenda Kibondo, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya
kampeni ya chama hicho katika majimbo manane mkoani hapa.
Zitto alisema ajali hiyo ilitokea saa mbili usiku na kabla ya kupinduka, gari hilo
lilipata pancha tairi moja la mbele likiwa
Msafara huo ulihusisha wagombea wote wanane wa majimbo ya Mkoa wa
Kigoma ambao unapita kila jimbo kufanya mikutano kwenye kata na jioni
hukutana kufanya mkutano katika eneo moja.
Dereva wa gari hilo alisema chanzo cha ajali ni pancha iliyotokea kwenye tairi la
mbele, upande wa kulia, na kusababisha ‘kumvutia’ porini na kupinduka.
Baada ya ajali hiyo iliyosababisha michubuko kwa watu wanne, majeruhi hao
walichukuliwa na kupelekwa mjini Kibondo kwa ajili ya kupatiwa huduma ya
kwanza na taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa waliendelea na ziara
katika Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo.
