Majambazi wavamia nyumbani kwa Nay Wa Mitego

Watu wanaodhaniwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa msanii wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego maeneo wa Kimara,jijini Dar wakati yeye akiwa safarini mkoani Arusha.

Nay alisema kuwa kwa muda wa wiki mbili yupo mikoani kwenye shughuli za kisiasa,siku ya tukio alipigiwa simu na wadogo zake kuwa usiku wa kuamkia juzi watu wasiofahamika walivamia nyumbani kwake wakiwa wameficha nyuso zao(wamevaa mask) wakati watu hao wakihangaika kukata nyaya za ‘fens’ alarm ikawa inapiga kila wakati.
‘’Unajua mie sipo Dar takribani wiki mbili nipo mikoani kwenye shughuli za kisiasa,wadogo zangu ndiyo wapo nyumbani kwangu walinipigia simu kuwa kuna watu wamevamia nyumbani usiku wa kuamkia juzi walikuwa wamevaa mask,sasa wakati wanahangaika kukata nyaya za fensi alam ikawa inapiga kelele ndipo wakaamua kupanda juu ya mstimu ili wakate umeme nyumba nzima ndiyo waingie,’’alisema Nay Wa Mitego.
Msanii huyo alisema baada ya majirani kusikia kelele waliamua kutoka nje na kuita kelele za mwizi ambapo majambazi hao walifanikiwa kukimbia wakiwa kwenye gari aina ya LandCruser nyeusi na taarifa za tukio hilo zimeripotiwa polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo