Njombe watangaza kula sahani moja na wavunjifu wa amani kwenye kampeni


Serikali Wilayani Njombe Imewataka Wananchi Kuendelea Kudumisha Amani Katika Maeneo Yao Katika Kipindi Hiki Cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu Pasipo Kusababisha Vurugu Katika Mikutano ya Kampeni.

Kauli Hiyo Imetolewa  na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba (pichani) Wakati Akizungumza na mtandao huu Ofisini Kwake Juu ya Mwenendo Mzuri wa Zoezi Kampeni Katika Wilaya ya Njombe.  

Aidha Dumba Amesema Pamoja na Taifa Kuwa na Zoezi Kubwa na Muhimu la Uchaguzi Mkuu Hapo Oktoba 25 Mwaka Huu Lakini Bado na Mambo Mengine Yanakwenda Kadri Inavyowezekana.

Pia Ametumia Fursa Hiyo Kuwataka Watanzania Wote Waliojiandikisha Katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Kuhakikisha Siku ya Kupiga Kura Wanajitokeza na Kupiga Kura Hiyo Kuwachagua Viongozi Wanaowataka.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Amesema Wao Kama Viongozi Ndani ya Taifa la Tanzania Wanaendelea Kuhakikisha Amani na Utulivu Vinakuwepo Muda Wote Kwa Maslahi ya Watanzania Wote Hususani Wazee,Wanawake na Watoto Ambao Mara Nyingi Huwa ni Waathirika Wakubwa Katika Matatizo Mbalimbali.

Kwa Upande Wake Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Lilisema Nalo Limejipanga Kikamilifu Ili Kuhakikisha Mchakato Huo Unakwenda Kama Ulivyopangwa Bila Kuingiliwa na Mtu Yeyote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo