Mabasi mawili ya Kampuni ya Zacharia Express mali
ya Pita Zacharia mkazi wa Tarime mjini yanayofanya safari zake
Tarime-Mwanza yameharibiwa kwa kupondwa na mawe kwa
kile kinachoelezwa ni ushabiki wa kisiasa.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alisema kuwa Octoba 26, majira ya saa tisa mchana katika kijiji cha sokoni,Kata ya Sirari,Wilayani Tarime
Gari lenye namba za usajili T.562 CAP aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Magazin ikitokea katika kituo
cha mabasi cha Sirari kuelekea katika egesho la kituo cha mafuta ilipigwa mawe.
Mambosasa alisema gari hilo lilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele,vioo vine vya madirisha
upande wa kulia na vioo vitatu vya madirisha upande wa
kushoto vyote vikiwa na thamani ya 6,500,000.
Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo majira ya saa sita mchana gari lingine lenye namba za usajili T.925
CZM aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Ezekia Merico(32) Dereva mkazi wa Isamilo Mwanza ilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo kimoja cha Dirisha la nyuma upande wa kulia
lenye thamani ya 2,000,000.
Mambosasa alisema kuwa Magari hayo ni mali ya Kampuni ya Zakaria Express, na kwamba
watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni Libaya Msabi (34)mkazi wa
Remagwe na Marwa Juma(17) mkazi wa Sokoni Sirari