Habari zilizotufikia hapa eddy blog usiku huu ni kwamba Waziri wa viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni huko India
Waziri huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Apollo nchini India
Siku chache zilizopita waziri Kigoda alizushiwa kifo katika mitandao ya kijamii jambo lililokanushwa vikali na serikali kupitia kwa masemaji wake Bw Assah Mwambene
Dkt Kigoda ni waziri wa pili kufariki katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baada ya waziri Celina Kombani naye kufariki dunia mwezi uliopita katika hospitali hiyo hiyo ya Apollo ya India alikokuwa akipatiwa matibabu