Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amekutana na wananchi na kupokea malalamiko ya migogoro ihusuyo ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam katika makao makuu ya wizara hiyo.
Siku ya jana waziri Lukuvi pia alipokea malalamiko ya wananchi katika manispaa ya kinondoni na hivi leo anapokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Temeke na Ilala.
