“Aliporudi kutoka kazini alianza kunishambulia kwa kunipiga kisha akaing’ata pua yangu na kumeza kipande cha nyama ya pua “ hayo ni malalamiko ya Mke wa Mr. Yang anayetokea kaskazini mwa nchi ya China katika mji wa Dezhou alipokuwa anatoa mashataka kwa maafisa wa polisi.
Mke huyo alisema alipokea kipigo toka kwa mume wake ambaye amedai alimpiga kisa hakupokea simu yake wakati alipokuwa kazini.
Kwa mujibu wa Madaktari wamesema Mke huyo alipata majeraha makubwa yaliosababisha atoke damu nyingi hivyo basi wanahitaji umakini mkubwa kufanikisha zoezi la upasuaji linafanikiwa.
Mpaka sasa Mwanaume aliyefanya tukio hilo anatafutwa na polisi baada ya kukimbia pasipo julikana.