Picha za uzinduzi wa Tanzania Media Foundation ulivyofana usiku wa kuamkia leo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo, Mama Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tanzania Media Foundation - Mfuko wa Habari Tanzania - TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. Mfuko huu unachukua nafasi ya Tanzania Media Fund 

Mkurugenzi wa Shirika la habari la Daraja Bw. Simon Mkina akipokea tuzo wakati wa uzinduzi huo wa Mfuko wa Habari Tanzania 


 Mkurugenzi wa TMF Bw. Ernest Sungura akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam






 Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyofanyika leo katika ukumbi wa Millenium Tower jijjini Dar Es Salaam.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TMF Mama Halima Shariff akitoa neno la shukurani baada ya bodi hiyo kuzinduliwa usiku wa kuamkia leo  katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. .

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana  Utamaduni na Michezo Mama Sihaba Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa Bodi ya TMF na  watendaji wa mfuko huo usiku wa kuamkia  leo katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na Edwin Moshi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo