Mshtuko: Katibu wa CCM afariki dunia

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Ernest Chale  amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es  Salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
 
Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya CCM kilisema kuwa  katibu huyo amefariki majira ya saa 5:30 asubuhi  jana katika  hospitali hiyo.
 
Alisema kuwa Jumatano ya wiki hii alikuwa anasumbuliwa  na ugonjwa wa  shinikizo la damu na Alhamisi alipelekwa katika Hospitali ya  Muhimbili na kulazwa wodi ya Mwaisela.
 
Alisema hali yake ilibadilika na hatimaye umauti ukampata.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma  Simba Gadafi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema Jumatano walikuwa wote kwenye kampeni na hali yake  ilibadilika usiku akiwa usingizini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo