Mr Nice ala sumu,....Yupo hoi hospitalini

Mr Nice ameponea chupuchupu kupoteza maisha baada ya kudai kula chakula chenye sumu

Kupitia ukurasa wake wa facebook Mr Nice ameandika: Mungu ni wakutumainiwa sana.maana atafanya atakalo yeye pale atakapotaka yeye na sii mwingine yoyote juu yake..food poison niliyopewa ilibidi leo 14/9/2015 watanzania muwe mkiongea lugha mbadala juu yangu hasa katika kuongeze jina langu kuwa refu kidogo(marehemu/hayati nk) lakini yesu wa nazarethi mama na babya yangu walisimama wima na kunifanya niendelee kupumua vyema hadi leo hii nimeweza kuandika sms hii kwa mikonoyangu mwenyewe tena .niko hosptl kwa muda wa wiki mbili sasa toka jumanne iliyopita mwanzo,naishukuru familia yangu,doctors waliopigania kuokoa roho yangu,mzee wangu mgombea james lembeli(kahama),jamaa na marafiki wote miliopigania uhai wangu . kampeni hizi za kisiasa jamani ni za muda tu inabidi tujue kuna maisha yanatakiwa yaendelee baada ya kampeni na uchaguzi na yanatakiwa yaendelee kwa upendo mmoja ,kuwekeana visasi kwa kuwa huyu anamkapenia fulani ama chama fulani hata mpaka tukafikishana katika hatua hii si jambo jema na mungu hapendezwi …..asante mungu asante yesu,naomba sana waandishi msithubutu kunipigia wala kunitafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hili tafadhali huwa sipendi “kick” kwa kupitia matatizo …nimeweka post hii kwa ajili ya kuwashukuru friends wangu wa fb na wale wote walioniombea coz siwezi kuwafikiwa wote mmoja mmoja … asante yesu asante mungu kwa kunitolea tena katika tundu la sindano…nimekuwa nikikumbana na mengi makubwa na kuyashinda kwa uwezo wako tu .14/9/2015


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo