Jamaa kakosea kutuma ujumbe ukaenda kwa Polisi ili apatiwe dawa za kulevya

William Lamberson raia wa Florida,Marekani amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kutuma ujumbe wa maneno kwa Polisi akidhani ni rafiki yake.

Ujumbe huo ulilenga kutaka apatiwe dawa za kulevya kutoka kwa rafiki yake huyo ambaye walikuwa wakishirikiana katika biashara hiyo lakini alikosea na kujikuta ukienda kwa  Brian Bergen ambaye ni kiongozi wa Polisi.
Polisi walianza kufanya uchunguzi wao na kugundua Lamberson anajihusisha na uuzaji wa dawa hizo hivyo baada ya uchunguzi aliwekwa ndani na kufunguliwa mashtaka ya kujihusiha na biashara hiyo haramu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo