Isikupite hii mpya kutoka kwa Dkt Magufuli

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amesema serikali ya awamu ya tano atakayoiunda baada ya uchaguzi mkuu wa October 25 iwapo atapata ridhaa ya watanzania, itatoa kipaumbele kwa sekta binafsi nchini kushiriki katika uchumi wa gesi na mafuta badala ya wageni ili kuliwezesha taifa kunufaika vya kutosha na sekta hiyo badala ya kuwachia wageni pekee kwa kuwa hakuna nchi inayoendelea bila kuwashirikisha wazawa katika maliasili zake lakini pia kuimarisha bandari ya Mtwara pamoja na ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka Mbambay.

Kauli hiyo ya Dr Magufuli ameitoa mkoani Mtwara wakati akizungumza na wakazi hao kwa nia ya kuomba kura ili aweze kuunda serikali ya awamu ya tano na kuongeza kuwa sekta binafsi nchini ina nafasi kubwa ya kuliwezesha taifa kupiga hatua za haraka za kimaendeleo iwapo itashirikishwa vya kutosha katika rasilimali mpya ya mafuta na gesi na kwamba serikali yake imedhamiria kuishirikisha sekta binfsi na hasa wazawa katika sekta hiyo.
 
Aidha Dr Magufuli ameongeza kuwa Tanzania ni nchi tajiri yenye rasilimali za kutosha na kwamba rasilimali hizo zikitumiwa vyema zinaweza kulifanya taifa kuwa nchi ya uchumi wa kati na kupunguza umasikini uliopo hivi sasa miongoni mwa watanzania na kwamba kinachohitajika na uongozi makini wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi na kwamba kazi hiyo inaiweza.
 
Akitokea wilayani Masasi kuelekea mjini Mtwara Dr Magufuli amezungumza na watanzania aliokuwa akikutana nao njiani lakini pia amefanya mikutano katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na baadae Mtwara mjini ambapo mmoja wa wagombea wabunge katika mkoa huo wa Mtwara amemtaka Dr Magufuli kuhakikisha Mtwara inakuwa na shule pamoja na vyuo vingi ili kuwawezesha wananchi kunufaika na rasilimali ya mafuta na gesi. 
 
Dr Magufuli tangu kuanza kwa ziara zake za mikoani kwa ajili ya kampeni ya kusaka urais ametembea zaidi ya kilomita elfu nne na mia saba kwa njia ya barabara kwa kile alichosema ni kutaka kujionea mwenyewe shida za watanzania badala ya kusimuliwa ili akipata ridhaa ya watanzania aweze kuzitatua.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo