Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kudadisi, kuchunguza na kuwapima wagombea kwa sera zao ili kuepuka kuchagua viongozi wabovu kwakuwa watanzania wanahitaji viongozi watakaoleta mabadiliko ya kidemokrasia na kuikwamua Tanzania katika wimbi la umasikini hali inaosababishwa na viongozi wachache wanaotumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe.
Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni za uchaguzi jimbo la Kahama mjini mbunge anayetetea nafasi yake kwa tiketi ya Chadema Mh.James Lembeli amesema wagombea wanaoomba kura kwakuwahonga wananchi hafafai huku akiwataka wananchi wa kahama kuchagua viongozi watakaoweza kufanya kazi ya kuleta maendeleo na sio kwenda bungeni kufanya mahesabu ya biashara zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kanda ya Serengeti Chadema Bw.Sylivesta Kasulumbai amesema hoja ya wasukuma sio kumuona Msukuma anaingia ikulu bali ni kumpata kiongozi muadilifu bila kujali kabila wala dini yake huku mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la kishapu Bw.Fred Mpendazoe akiwataka watanzania kudadisi,kuchunguza na kujiuliza kwanini viongozi wakubwa wa chama cha mapinduzi wanatoka na kuhamia vyama vingine.