Taarifa zilizotufikia muda huu kwenye chumba chetu cha habari ni kwamba Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu
Taarifa hizo zimesema Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu
Marehemu Kombani alikuwa akiugua saratani
Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu uliowapata
Taarifa zaidi za msiba huo zitakujia hapa hapa