Baada ya mgogoro na mgomo uliodumu kwa zaidi ya miezi minne kati ya chuo kikuu cha Kampala na wanafunzi wa kozi ya famasia kutokana na kutokuwa na usajili serikali imekipa usajili wa muda ili kuondokana na mgogoro huo.
Afisa uhusiano wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Nsachris Mwamwaja amesema uamuzi huo umefikiwa na bodi ya baraza la famasia ili kusaidia wanafunzi wanaomaliza kozi hiyo waweze kutambuliwa katika soko la ajira.
Baadhi ya wanafunzi waliokumbwa na seke seke hilo wameitaka serikali kuhakikisha inafanya ukaguzi kwenye vyuo kujiridhisha kama kozi zote zimesajiliwa ili kuepusha migogoro kama hiyo.
Kwa upande wa uongozi wa chuo hicho wamesema mgogoro huo umesababisha madhara kadhaa ikiwemo uharibifu wa mali na kutoa wito kwa serikali.