Watu 150 waliokuwa wakishiriki sherehe za hija wamefariki kwenye mkanyagano uliotokea katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, maafisa nchini Saudi Arabia wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema kupitia Twitter kwamba watu wengine 400 wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea mji wa Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.
Shughuli za uokoaji zinaendelea, idara hiyo imeongeza.
Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Adha.
UPDATE: Idadi ya watu waliofariki hadi sasa katika sherehe za kumaliza hijja huko Mecca imefikia watu 310 na majeruhi ni 450.
UPDATE: Idadi ya watu waliofariki hadi sasa katika sherehe za kumaliza hijja huko Mecca imefikia watu 310 na majeruhi ni 450.
chanzo:bbc