Mwalimu akiona cha moto baada ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wake

Nchi nyingi duniani kote ikiwemo Tanzania sheria ya mtu kuvuka umri wa kuitwa mtoto, hadi afikishe umri wa miaka 18 na kuendelea ndio inaaminika kuwa ni mtu mzima, ila mtu aliye chini ya miaka 18 haruhusiwi kutumia vitu kadhaa kama pombe, kujihusisha katika mahusiano ya kimapenzi hususani na mtu aliyemzidi umri.

Licha ya kukiri kufanya kosa la kutembea na mwanafunzi wake mwalimu Caroline Berriman amehukumiwa kwenda jela. Caroline Berriman ambaye alikuwa ni mwalimu wa darasa msaidizi katika shule ya Abraham Moss Community, alishitakiwa kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi wake aliye na umri wa miaka 16.

Caroline Berriman ambaye ana umri wa miaka 30 kwa sasa, alishitakiwa kwa makosa mawili ya kufanya mapenzi na mtoto na kutenda kosa hilo katika sehemu inayoaminiwa na watu.
Caroline Berriman ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya Abraham Moss Community iliyoko jijini Manchester, shule ambayo ina wanafunzi 1600 wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 16 wa shule ya msingi na sekondari, amehukumiwa kwenda jela miaka miwili, kufanya kazi za kijamii za bila malipo kwa muda wa masaa 250 pamoja na kulipa pound 100 kama fidia kwa muhanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo