Zaidi ya wanachama 100 wa CCM warudisha kadi na kutimkia CHADEMA Bukoba

Zaidi ya wanachama miamoja akiwemo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Bukoba jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani wa kata ya kahororo Chief Kalumuna wamerejesha kadi za chama cha mapinduzi na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei amesema wanachama hao ambao wengiwao wamepelekea kadi hizo kimyakimya kwa muda wa siku saba na kufikia wanachama miamoja hamsini wameamua kufanya hivyo kwaajili ya kumuunga mkono waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa na kuhakikisha anapata kiti urasi amwamu ya tano kupitia chama hicho. 
 
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapindi jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani anae maliza muda wake katika kata ya Kahororo Chiefu Kalumuna amesema yeye amekuwa mpinzani ndani ya chama kwa kipindi kilefu na sasa ameamua kukihama chama chake kutokana na uonevu pamoja na mabavu yanayotumiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwakukata majina ya wanachama wanokuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi ili wasigombee nafasi mbalimbali za uongozi hatakama wanakulika na wananchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo