Wanachama wa CCM waandamana kupinga uteuzi wa mgombea ubunge

Mamia ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo.

Tukio hilo limekwenda samabamba na mwenyekiti wa zamani wa umoja wa viaja wa CCM mkoa wa Kigoma Edgar Mkosamali aliyegombea na kushika nafasi ya nne, kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT wazalendo, baada ya CCM kumteua Atashasta Nditiye aliyeshika nafasi ya tatu kuwania ubunge katika jimbo hilo, ambapo wanachama hao ambao hawakuridhika na maamuzi wamelazimika pia kurejesha kadi zao na kujiunga na upinzani.
 
Viongozi wa CCM walipata kazi ya ziada kuwatuliza wananchama hao, ambapo waliwataka kukubaliana na maamuzi ya halmashauri kuu ya taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo