Zaidi ya abiria miamoja hamsini waliokuwa wakisafiri na meli ya Mv Serengeti inayofanya safari zake kutoka Mwanza hadi Bukoba wamenusurika kifo mara baada ya meli hiyo kukumbana na upepo mkali na kushindwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba.
Meli hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Mwanza kuelekea mjini bukoba ambapo ilikumbana na upepo mkali ndandi ya ziwa victoria na kushindwa kutioa nanga katika bandali ya Bukoba nakupelekea nahodha wa meli hiyo kuirudisha majini mpaka upepo ulipo tulia ndipo ilifanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba majira ya saa tano asubuhi.
Wakizungumza mara baada ya meli hiyo kutia nanga katika bandari ya Bukoba baadhi ya wananchi wamesema meli hiyo ilianza kuyumba majini majira ya saa kuminamoja alfajiri hali ambayo imewatia wasiwasi ambapo wamekaa majini kwa zaidi ya saa sita ndipo walipofanikiwa kutoka majini huku wakiwa wanahali mbaya kisaikorojia.
Kwa upande wake nahodha wa meli hiyo Bembele Mwita amesema kuwa meli hiyo ilikuwa haina tatizo lolote la kiufundi bali upepo mkali ulikuwepo ndani ya ziwa Victoria ndio ulichangia kwa kiasikikubwa na kukwamisha meli hiyo na kushindwa kutioa nanga katika bandari ya Bukoba.
Nitakribani miezi miwili imepita meli ya Mv Serengeti ianze kufanya kazi kama mbadala wa meli ya Mv Victoria baada ya kusimamishwa kwa ajili ya matengenezo.
