Walinzi wauawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao idadi yao haikuwza kufahamika mara moja wamevamia kituo cha mafuta cha State Oil kilichopo eneo la Kisasa manispaa ya Dodoma na kuua walinzi wawili wa kituo hicho kisha kupora fedha taslim shilingi milioni kumi na pamoja na vitu mbalimbali na kutokomea pasipo julikana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi David Misime amesema majambazi hayo yalivamia kituoni  hapo usiku na kuwashambulia walinzi kwa kiwapiga na kitu kizito vichwani mpaka kupoteza maisha na kisha kuvunja kontena lililokuwa na shehena ya vifaa vya ujenzi na kuiba vitu mbalimbali pamoja na fedha taslimu shilingi milioni kumi.
 
walinzi waliouwawa kwenye tukio hilo wametambulika kwa majina ya Paulo Nduluma na Aloyce Patsango wote wakiwa ni jamii ya wamasai huku kamanda Misime akiiasa jamii hasa wale wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu watambue kuwa uhalifu mwisho wake ni kuishia kwenye mikono ya dola.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo