Baadhi ya Wakulima katika Bonde la UYOLE lililopo nje kidogo ya Mji wa MBEYA wameanza kunufaika na Mradi wa Umwagiliaji maji wa IGANJO.
Miundombinu ya mradi huo imejengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 190.
Mwenyekiti wa Ushirika wa Umwagiliaji Maji Bonde la UYOLE - JOHN SODA amesema kuwa ujenzi wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 na asilimia 20 zilizobaki zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Utekelezaji wa mradi huo wa Umwagiliaji maji wa IGANJO umelenga zaidi kilimo cha zao la Viazi Mviringo na Mbogamboga.