Wagombea wa CCM wapinga matokeo ya kura za maoni

Wagombea wa ubunge katika kura za maoni kupitia tiketi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigoma Kusini yaliyotagazwa na Katibu Msaidizi wa Chama Wilaya ya Uvinza, wamepinga matokeo ya kura ya maoni zilizofanyika hivi karibuni.

 Kutokana na hali hiyo, wagombea hao wameamua kumwandikia Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, kueleza malalamiko yao hayo.
 
Barua kwenda kwa Kinana iliandikwa Agosti 5, mwaka huu na nakala kutumwa kwa Katibu wa CCM Wilaya, Katibu Mkoa ikiwa imesainiwa na wagombea sita kati ya 13 wakiwa na sababu kadhaa.
 
Katika barua yao, wagombea hao walisema sababu za kupinga matokeo hayo ni vituo vya kata ya Kalya kuwapo na idadi kubwa ya wapiga kura licha ya awali kuandika barua ya kulalamikia kwa viongozi Julai 26, mwaka huu bila kuchukuliwa hatua.
 
Walisema sababu nyingine ni kuwapo kwa idadi kubwa ‘feki’ iliyotayarishwa kabla ya uchaguzi hasa katika tawi la Kabukuyungu ambako idadi ya wapiga kura isiyohakikiwa ilikuwa 648, wakati baada ya matokeo kutangazwa ilionyesha Manju Msambya, alipata kura 300 na Salum Sasilo (1,305).
 
Aidha, walisema sababu nyingine ni mgombea Jumanne Muhitira, alilazimishwa kujitoa wakati wagombea wakiwa Ilagala baada ya kushindwa kukamilisha malipo, lakini alipigiwa kura baada ya kamati ya siasa kuliweka jina lake.
 
Aidha, walisema sababu nyingine ni viongozi wa msafara kumuachia mgombea Hasna Mwilima, kutumia gari la msafara usiku kucha wakati wagombea walipokuwa kata ya Sigunga kufanya kampeni na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
 
Wagombea waliosaini barua hiyo ni Msambya, Waziri Mourice, January Kizito, Idd Ndabhona, Dismas Malele na Norbet.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo