Waandishi wa habari wapigwa mawe mkoani Ruvuma

Tukio hili la wanahabari kupopolewa kwa mawe, liliripotiwa kutokea  katika kijiji cha Ruanda kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani  Ruvuma Agosti 17, mwaka huu ambako walikwenda kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Imeelezwa kwamba baada ya kufika katika kijiji hicho, kundi la watu waliokadiriwa kufikia 40, walianza kuwashambulia wanahabari hao kwa mawe.
 
Katika tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Ruanda, Deogratias Haule, aliyekuwa amefuatana na wanahabari hao, pia alishambuliwa kwa mawe na kumsababishia majeraha puani na mdomoni na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, amekiri kutokea kwa tukio hilo lililotokea majira ya mchana.
 
Kamanda Msikhela aliwataja waandishi wa habari waliokumbwa na mkasa huo kuwa ni Kassian Nyandindi, wa magazeti ya kampuni ya Business Times, Aden Mbelle na Pastory Mfaume, kutoka Redio  Jogoo FM ya mjini Songea mkoani Ruvuma.
 
Alisema wanahabari hao walipatwa na mkasa huo baada ya kwenda kutekeleza majukumu yao ya kikazi ya kuandika tukio la kufungwa kufuli ofisi za kata ya Ruanda, kitendo kilichofanywa na baadhi ya wanakijiji hicho wasiofahamika.
 
 Kamanda Msikhela alisema baada ya wanahabari hao kukamilisha shughuli yao iliyowapeleka, ghafla liliibuka kundi la watu hao na kuanza kuwashambulia kwa mawe wakati wakijiandaa kurejea mjini Songea ambapo mmoja wa waandishi hao, alirushiwa jiwe usoni. 

mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo