Mtoto wa miaka 3 aliyepotea kiajabu aokotwa pangoni jijini Mwanza

Mtoto wa miaka mitatu, Zainabu Adam, ameokotwa katika pango lililopo Mabatini Mtaa wa Nyerere A uliopo jijini Mwanza, baada ya kupotea nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha.
 
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Hassan Maulid, alisema mtoto huyo alikutwa kwenye korongo hilo baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kusikia sauti yake wakati akilia. 
 
“Tulipeleka taarifa kituo cha polisi Mabatini kuhusiana na kelele hizo, tuliongozana hadi eneo la tukio na waokoaji walizama ndani na kumuokota mtoto huyo.
 
Alisema walimpeleka kituo cha polisi mkoa wa Mwanza na kupatiwa PF3 na kumpeleka hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa afya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo