UKAWA wajigamba kuifunika CCM

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimepanga kufanya uzinduzi wa aina yake wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu katika tukio lililopangwa kufanyika katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Umoja huo utatumia fursa hiyo kumkabidhi mgombea wake wa nafasi ya urais katika uchaguzi huo, Edward Lowassa, ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 na pia kutangaza mambo ambayo serikali yake itayasimamia endapo Watanzania watawapa ridhaa ya kuliongoza taifa.


Mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji, aliwaambia wananchi katika maeneo yote walikopita jijini Dar es Salaam kuwa mtu anayetaka kuona nguvu ya upinzani inabidi asubiri kuona wakati wa uzinduzi.


“Kama CCM inadhani hatujajiandaa vizuri, sasa ngojeni muone siku ya uzinduzi wetu wa kampeni na hapo ndipo mtakapoona tulivyojipanga. Mnaounga mkono Ukawa mje kwenye uzinduzi katika siku itakayotajwa,” alisema Duni aliyehama kutoka CUF na kujiunga na Chadema ili awanie nafasi ya Makamu wa Rais.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa Chadema aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa maelezo kuwa yeye si msemaji rasmi wa Ukawa, alisema kitakachotokea kesho Jumamosi ni zaidi ya “mafuriko na Tsunami” iliyokuwepo wakati wa uzinduzi wa CCM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo