BAVICHA waitaka serikali kutenda haki

Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA), limeitaka serikali kutenda haki katika kipindi chote cha kampeni na kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi alisema kuwa kumekuwa na vitendo vya wazi vinavyofanywa na serikali ya CCM ili kudhoofisha nguvu ya Ukawa kushika dola, jambo ambalo halikubaliki.



Katambi alisema kuwa hata Agosti 29, siku ya uzinduzi wa kampeni ambayo mgombea kupitia Ukawa, Edward Ngoyai Lowassa anatarajiwa kuunguruma ilikuwa ikifanyiwa mizengwe, jambo ambalo si zuri katika siasa zinazofuata misingi ya kidemokrasia.





Naye Katibu Mkuu Bavicha wa Taifa, Julius Mwita alisema imegundulika kuwa kuna njama kabambe zimeandaliwa ili kudhoofisha nguvu ya Ukawa na hali hiyo haitavumilika.



“Tunaomba kufanya zoezi zima la kampeni kulingana na sheria za uchaguzi zinavyosema na si kukandamizana na wakati mwingine kutumia vyombo vya dola,” alisema Mwita.



Akizungumzia ufunguzi wa kampeni Agosti 29, katibu huyo alisema kuwa hata kama serikali haitatoa ulinzi wao wako imara na kuongeza kuwa kikosi cha Red Briged na Blue Guard viko imara kusimamia shughuli zote za ulinzi katika mkutano huo.



Kiongozi huyo aliongeza kuwa, siku ya ufunguzi hakutakuwa na mafuriko bali kutakuwa na maporomoko ya watu kitu ambacho hata dunia nzima itashangaa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo