UKAWA Singida waanza kumegana wao kwa wao

Chama cha CUF wilayani Ikungi kimekilalamikia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Singida kwa kuweka wagombea udiwani wote wa wilaya hiyo na kukiuka utaratibu wa UKAWA wa kusimamisha mgombea anaye kubalika bila taarifa yeyote.

Akiongea katika kikao cha viongozi wa CUF na wagombea udiwani wa chama hicho katibu wa CUF wilaya ya Ikungu Bwana Selemani Ntandu amesema tokea tarehe kumina tatu mwezi huu baada ya vyama vya siasa kutia saini makubaliano ya mgawano katika kata yeye mpaka sasa haja pata taarifa yeyote na kushutukia Chadema wamesha chukuwa fomu za kugombea. 
 
Baada ya kubaini hivyo  mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ikungi na mjumbe wa baraza kuu la uongozi wa CUF taifa Bwana Athumani Hengu amesema CUF wilayani Ikungi wamefanikiwa kuungwa mkono katika kata nyingi na kupata wawakilishi wa udiwani karibu kata zote.
 
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Singida Bwana Shabani Hamisi Limu nayeye amesema CUF wilayani Ikungi hawakuwa wamejiandaa kwenye uchaguzi wa udiwani na kutokana na hali hiyo wao Chadema iliwalazimu madiwani wao wote kuchukuwa fomu za kugombea, kwa hiyo malalamiko yao siyo ya msingi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo