WAKAZI wa Halmashauri ya mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka kumi sasa hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu.
Wakizungumza na eddy blog wakazi hao wamesema licha ya eneo hilo kuwa jirani na vyanzo vya maji kama mto Ruaha lakini ni zaidi ya miaka kumi sasa wameendelea kukumbwa na adha ya ukosefu wa maji hali ambayo wamesema inahatarisha maisha yao.
Kwa upande wake mdau wa maendeleo na mkazi wa Kilolo, Bw. Venance Motto anasema tatizo ni kubwa na kuitaka serikali kuona umuhimu wa kuchukua juhudi za kulimaliza.