Katika Jimbo la Makete, yaliibuka madai ya dosari kadhaa hali iliyomfanya Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike, kusema kuwa changamoto za miundombinu katika jimbo hilo zimesababisha kuchelewa kwa matokeo ya ubunge.
Katika uchaguzi huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge alipata kura 8,534 huku mpinzani wake wa karibu, Profesa Norman Sigala akipata kura 8,211, Bonic Muhami 500, Fabianus Mkingwa 466 na Lufunyo Rafael 226.
Hata hivyo, Profesa Sigala alipinga matokeo hayo kwa kuwasilisha malalamiko yake kwa vikao vya juu ambavyo jana vimetoa uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo utafanyika kesho Agusti 13