Rais Kikwete ampigia saluti Dkt John Magufuli

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete ameipongeza sekta ya ujenzi kwa kuondoa aibu kwa watanzania kulazimika kupita nchi jirani wakati wa kusafiri kutoka mkoa moja kwenda mwingine ndani ya nchi huku akiweka wazi kuwa akistaafu maskani yake yatakuwa kijijini Msoga,Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais Kikwete ameyasema hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam katika hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na taasisi pamoja na idara zilizopo chini ya wizara ya ujenzi na kuongeza kuwa serikali yake iliweka kipaumbele katika sekta ya ujenzi kwa makusudi kwa kuwa usafirishaji ndio nguzo kuu ya kukuza uchumi huku akiipongeza wizara ya ujenzi kwa kuliondolea taifa aibu ambapo watanzania walilazimika kupita nchi jirani wakiwa safarini kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kutokana na ubovu wa barabara.
 
Aidha rais Kikwete mbali ya kuelezea namna sekta ya ujenzi inavyochangia kukuza uchumi wa nchi na kuondoa umasikini hakusita kummwagia sifa kem kem waziri wa ujenzi Dr.John Pombe Magufuli huku akimuelezea kuwa ni mchapa kazi makini asiyeyumbishwa na rushwa na kwamba moja ya wizara ambazo hazikumnyima usingizi wizara ya ujenzi ni miongoni mwao.
 
Waziri wa ujenzi Dr.John Pombe Magufuli kwa upande wake ameelezea namna Tanzania ilivyopiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kujenga miundo mbinu ya barabara ambapo zaidi ya kilomita 17 elfu zimejengwa kwa kiwango cha lami kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha zake za ndani lakini pia namna sekta ya ujenzi ilivyosaidia kukuza uchumi wa nchi.
 
Pia maafisa watendaji wakuu waa idara na taasisi mbalimbali zilizopo chini ya wizara ya ujenzi walipata fursa ya kuelezea mafanikio yao mbele ya rais Kikwete ambapo afisa mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini Tanroads mhandisi Patrick Mfugale amesema ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 mikoa yote nchini itakuwa imeunganishwa kwa barabara za lami  na kuelezea  sababu za kitafiti zinazofanya barabara nyingi hapa nchini hazidumu kwa muda mrefu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo