Maelfu ya wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Arusha wamejitokeza kumpokea na kumsikiliza mgombea urais wa CHADEMA kupitia UKAWA na waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowasa huku wakiwapokea wanachama wa (CCM) na viongozi akiwemo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh.Laurence Masha.
Wengine waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na katibu wa CCM wa wilaya ya babati Bw,Daniel Porokwa,Mwenyekiti wa UWT,wa wilaya ya karatu bi fabiola manimo katibu wa UWT wa wilaya ya Siha,na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha kwa zaidi ya miaka 20 Mh.Yona Nnko.
Pia Mwenyekiti wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha Bw.Robson Naitinyiku,aliyegombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na kushika nafasi ya pili Bw.Lenana Lenganasa,Diwani wa kata ya Ruvu Remiti wilayani Simanjiro Bw,Siyoi Solomoni sumari na kiongozi mkuu wa ukoo wa ukoo wa nanyaro kutoka Arumeru Mashariki.
Baada ya kazi ya kuwapokea wanachama wapya kukamilika viongozi wa ngazi mbalimbali wa UKAWA akiwemo muasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtey wakatoa salam huku wakiendelea kuwataka watanzania kupokea mabadiliko na kuhakikisha kuwa yanafanyika kwa amani.
Ukafika wakati wa mgombea urais wa CHADEMA kupitia umoja wa UKAWA Mh.Edward Lowasana mgombea Mwenza Mh.Duni Haji ambao wameendelea kuwataka wananchi kudumisha umoja na ushirikiano ili waweze kushinda uchaguzi na kupata nafasi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayowakabli wananchi.