Prof. Norman Sigala azungumzia Mahusiano yake na Dkt Binilith Mahenge baada ya kura za maoni

Baada ya kumalizika kwa kura za maoni kupitia Chama cha mapinduzi CCM jimbo la Makete mkoani Njombe, imeelezwa kuwa chama hicho hakina mpasuko tangu wilaya ya Makete ianze hadi hivi sasa

Hayo yamesemwa na mgombea ubunge jimbo la Makete kupitia chama cha Mapinduzi CCM Prof. Norman Sigala King wakati akihojiwa moja kwa moja na kituo cha redio Kitulo FM wilayani Makete jana

Prof. Sigala amesema katika chama chake hakuna mpasuko na badala yake kuna tofauti ndogondogo za hapa na pale zilizotokana na kura za maoni, na hizo zipo ndani ya wafuasi wa waliokuwa wagombea katika kinyang'anyiro ambacho yeye ameibuka mshindi

"tangu CCM ianze hapa Makete hakujawahi kutokea mpasuko, kuna tofauti ndogondogo tu tena za kawaida zilizotokana na uchaguzi wa kura za maoni na hizo zipo kwa wafuasi wetu na sio sisi" amesema Prof Sigala

Kuhusu uhusiano wake na Mbunge aliyemaliza muda wake Dkt Binilith Mahenge, Prof Sigala amesema wana mahusiano mazuri mpaka sasa na wamekuwa wakishauriana mambo mbalimbali tofauti na watu wanavyodhani

"Dkt Mahenge ni kaka yangu, tunawasiliana vizuri tu, na hata hivi leo tunacheka, na amekuwa akinibeba kwenye gari yake kunipeleka benki kuchukua fedha, sina ugomvi wala tatizo na Dkt Mahenge" amesema Sigala

Aidha amewataka wanamakete kuondoa tofauti zao na kujiandaa ipasavyo kupiga kura ili wamchague kiongozi anayewafaa, huku akiwasisistiza wanachama wa CCM kuusaka ushindi kwa ngazi zote kuanzia diwani mpaka Rais


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo