Polisi yapiga marufuku vikundi vya Ulinzi vya vyama

Wakati kampeni za uchaguzi mkuu wa kuwapata madiwani, wabunge na Rais zikianza rasmi kesho, Jeshi la Polisi limepiga marufuku vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa ambavyo imevielezea kuwa na  mwelekeo wa kijeshi.

Polisi imevielezea vikundi hivyo vya Green Guard cha chama cha mapinduzi, Red Briged cha Chadema na Blue Guard cha Chama cha Wananchi CUF, havipo kisheria na vimekuwa vikiingilia majukumu ya jeshi la polisi.


Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es salaam, Kamishna wa Polisi, Operesheni na Mafunzo, PAUL CHAGONJA amevionya vyama vya siasa kuwa kuendelea kumiliki vikundi hivyo ni uvunjifu wa sheria na hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa kwa chama chochote kitakachoendelea kukaidi amri hiyo.

Pia polisi imepiga marufuku Maandamano ya kuelekea kwenye mikutano ya kampeni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo