Mgombea Ubunge wa CCM aahidi mshahara wake wote atawapa wananchi wake


Mgombea Ubunge  kupitia tiketi ya chama  cha Mapinduzi “CCM” jimbo la Rungwe Mkoani Mbeya  Sauli Amon, amesema ikiwa atapata  ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo hilo, mshahara wake wote wa ubunge utaingia kwenye akauti ya elimu ya Wilaya ya Rungwe, ili kusaidia shughuli za maendeleo.

Akizungumza na eddy blog team kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Rungwe, mara baada ya kurejesha fomu mgombea huyo amesema ikiwa atachaguliwa, atafanya kazi kwa kuzingatia ilani ya chama  cha Mapinduzi, pamoja na vipaumbele vyake ambavyo ni pamoja na kuboresha huduma za afya kwa kusomesha madaktari.

Aidha Mgombea huyu pia amesema ataondoa changamoto ya wana Rungwe ya kuuza ndizi zikiwa changa,na kuwa na mfumo wa uuzaji wa ndizi  ghalani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo