Hili ni tukio ambalo limechukua sana headlines mitandaoni na kwenye Vyombo vya Habari vikubwa vya Kimataifa Duniani, mtangazaji kavamiwa akiwa anarekodi show yake kwenye Kituo cha Radio Brazil !!
Kinachoibua maswali kwa upande mwingine ni kuhusu nani kahusika na mauaji hayo? wauaji waliingia mpaka ndani na kuua alafu wakafanikiwa kutoka salama, mtangazaji Gleydson Carvalho kauawa kwa kupigwa Risasi tatu kichwani na kifuani.
Wauaji hao walivamia na kumzidi nguvu mtu wa mapokezi, wakamkamata producer wa show akalazimishwa kuingia chini ya meza… alafu wakamalizia kwa kumuua mtangazaji huyo ambaye alikuwa maarufu sana kutokana na kuikosoa Serikali kushindwa kupambana na tatizo la Rushwa.
Angalia video hii
Angalia video hii
