Mrema aomba wapiga kura wake wasimpige chini ili amalizie ahadi zake

Mgombea urais wa chama cha Tanzania Labour Party(TLP) Bw.Macmillan Lyimo amezindua kampeni ya uchaguzi wa chama hicho kitaifa  mkoani Kilimanjaro na kusema ilani ya chama hicho ni kupambana na umaskini pamoja na kulinda raslimali zilizopo hapa nchini ili ziwanufaishe wananchi na siyo watu wachache.

Akizungumza na wana chama wa chama hicho kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya njiapanda himo wilaya ya Moshi mgombea urais Macmillani Lyimo amewataka watanzania kuwa makini na uchaguzi wa mwaka huu kwa kuchagua viongozi wenye uzalendo na Tanzania.
 
Amesema uchaguzi wa mwaka huu siyo wa Tanzania pekee bali ni uchaguzi wa dunia kutokana na uwepo wa mataifa makubwa yanayotamani kuvuruga amani iliyopo hapa nchini ili kuweza kumiliki raslimali zilizopo Tanzania kama madini na mafuta.
 
Naye mwenyekiti wa chama cha TLP Mh.Agustino Mrema ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la vunjo amewataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua ili aweze kukamilisha ahadi zake za ujenzi wa barabara za lami ukanda wa tambarare.
 
Naibu katibu mkuu wa chama hicho Bi Dominatha Rechungura amesema wananchama wa chama hicho wana imani na mgombea uraisi kwa tiketi ya TLP Bw. Macmilan Lyimo na kuwataka wananchi wa jimbo la vunjo kupuuza kauli za watu wanaombeza mwenyekiti wa chama hicho kuwa ni mgonjwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo