Mrema achukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Vunjo


Mgombea ubunge jimbo la vunjo  
kupitia chama cha TLP Agustino Mrema (kushoto) akipokea fomu ya kugombea 
ubunge katika jimbo la vunjo kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya 
moshi vijijini FOLGENCE MPONJI(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

MGOMBEA ubunge jimbo la Vunjo  
na mwenyekiti wa chama cha TLP ,Agustino Lyatonga Mrema ametamba kuwa  
jimbo hilo ni mali yake na hayuko tayari kuona likichukuliwa na
Ukawa.


Mrema alitoa kauli hiyo wakati  
akiongea na mamia ya wafuasi wa chama hicho muda mfupi baada ya kuchukua 
fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi cha halmashauri ya wilaya ya  
Moshi Vijijini.

Mrema alisema kuwa jimbo la  
vunjo ni mali yake na hayupo tayari kuliacha lichukuliwe na
 ukawa 
 
Alisema amelazimika kuchukua  
fomu ya kugombea jimbo hilo kutokana na maombi ya wananchi wa jimbo la  
vunjo wengi wao wakiwa wanawake ambao muda mwingi walikuwa wakimfuata  
nyumbani kwake wakimtaka agombee kutokana na rekodi nzuri aliyo watendea 
kipindi kilicho pita,

 
Hata hivyo alieleza kuwa  
propaganda zinazo enezwa na wapinzani wake wakidai kuwa yeye amezeeka na 
ni mgonjwa, nizakupuuzwa kwani kwa sasa yeye ana afya njema na anataka  
aitwe ‘bebi’ huku akionya kuwa wanao tumia sera ya uzee na ugonjwa kwa  
lengo la kumwangusha kamwe hawatafanikiwa kwani wananchi wa vunjo pamoja 
na mkewake ,Rose Mrema ndio wenye kujua utendaji wake wa kazi na hivyo 
wahitaji  kuchaguliwa mtu mwingine.


“ Mengi yamesemwa kuwa mrema 
hagombei ni mzee ni mgonjwa hivi mkiniona mimi ni mzee jamani ,mimi ni 
bebi ,uzee mwisho Chalinze ,waliokuwa na wasiwasi eti sigombei .sasa 
nagombea afya yangu imeimarika na hao ukawa wataisoma namba mwaka 
huu”alitamba Mrema

Mrema alisema kuwa kazi aliyo 
ifanya katika kipindi chake cha ubunge inaonekana na amejipanga 
kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wananufaika zaidi na juhudi zake  
kwakuwa amekuja na kasi mpya ya kuwaletea maendeleo na tayari amenunua  
gari la kusafirisha abiria  (coster) linalotumika katika jimbo hilo  
kusafirisha wakina mama wajawazito, shughuli za misiba pamoja na kubeba 
wananchi katika maeneo yao bila kuwatoza malipo yoyote  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo