Mpya tena, kuhusu Matokeo ya Ubunge CCM wilaya ya Makete

Ishu ya matokeo ya kura za maoni ya Ubunge jimbo la Makete kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) imechukua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa matokeo yatabaki vile vile kama yalivyotangazwa awali na si vinginevyo

Taarifa tulizozipata ni kwamba matokeo yaliyotangazwa awali yamefutwa na kura zitahesabiwa na matokeo kutangazwa upya lakini hali imekuwa tofauti na hivyo

Akizungumza na eddy blog kwa njia ya simu mkurugenzi wa uchaguzi CCM wilaya ya Makete Bw. Salum Choni amesema hakuna matokeo yanayotangazwa mara mbili

"Umeshaona wapi matokeo yakitangazwa mara mbili? yale yaliyotangzwa yatabaki hivyo hivyo kwa kuwa hakuna matokeo yanayotangazwa mara mbili" amesema Choni

Matokeo yaliyotangazwa awali yalionesha kuwa mgombea anayetetea nafasi yake Dkt Bililith Mahenge aliibuka mshindi na kuwabwaga wagombea wanne aliokuwa akichuana nao

Hali hiyo iliibua gumzo na kusababisha wananchi kufurika kwenye ofisi za CCM wilaya kutoa manung'uniko yao kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa jambo ambalo limekanushwa na mkurugenzi wa uchaguzi huo na kusema haki imetendeka kwa wagombea wote


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo