Benki kuu ya Tanzania (BOT) kanda ya kati imesema kuwa kuanzia leo Agosti 6 itabadilisha fedha zilichakaa kwa wakazi wa kanda hiyo kwenye banda lao la maonyesho lililopo kwenye viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Hayo yamesemwa na Mchumi kutoka BOT kanda ya kati Dk, Zegezege Mpemba wakati akizungumza kwenye banda lao la maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayoendelea katika viwanja vya nanenane vilivyoko mjini hapa.
Dk, Mpemba amesema kuwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya kati inayosimamiwa na BOT inakabiliwa na tatizo la noti chakavu ambazo hawajuwi mahali pa kuzipeleka na kuwataka kuziwasilisha katika banda hilo Agosti 6 mwaka huu ili ziweze kubadilishwa.
Kwa upande wake Dominic Mwita ambaye pia ni mchumi wa BOT amewataka wananchi kufika kwenye maonyesho hayo ili waweze kujua ni namna gani wanavyofanya kazi
