Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima , amesema kuwa kura za maoni zilizopigwa jimboni humo hazikuwa huru na haki kwa madai kwamba waliopiga kura walikuwa wachache lakini kura za matokeo zikawa nyingi.
Amekuwa nafasi ya pili kwa kupata kura 8, 212 na mshindi wa kwanza kapata kura 16, 294
“Mchakato uligubikwa na udanganyifu mkubwa, kura haziendani na uhalisia, pia mawakala hawakutia saini baada ya kumalizwa kwa upigaji kura katika vituo vyao, lakini ninaviachia vikao vya maamuzi vifanye kazi yake,” alisema Malima.
