Kiongozi huyu wa CHADEMA atimkia ACT - Wazalendo

Aliyelkuwa katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika wilayaya Butiama Bw Richard Choge Magori amekihama chama hicho kisha  kuijunga na chama cha ACT wazalendo kabla ya  kuteuliwa kwa ajili ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Butiama mkoani Mara.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu na mkurugenzi wa wilaya ya Butiama kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi ili kumwezesha kugombea ubunge katika jimbo hilo, kada huyo mpya wa chama cha ACT- wazalendo, amesema kuwa ameamua kujiunga na chama hicho na kugombea ubunge katika jimbo hilo baada ya kubaini wanachama 
walipendekezwa kugombea ubunge katika jimbo hilo mh Nimrod Mkono wa CCM na Bw Yusuf Kazi wa chadema hawana uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi wa jimbo hilo jipya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo