Mbowe: Tunaamini tulianza na Mungu kwenye safari yetu, tunaimani tunaendelea na mungu na tutamaliza na mungu
Mbowe: Tunaamini kila linalotokea ni mpango wa Mungu.
Mbowe: Tumepigana kwa miaka 25 kufika hapa tulipo leo, haikuwa kitu rahisi, wapo waliopata matatizo mengi.
Mbowe: Lakini wako tuliowaita magamba, nao wakaamua kimagamba magamba wakafunga safari yao ya matumaini kutafuta haki
Mbowe: Tuna kila sababu ya kuwaunga mkono, tuna kila sababu ya kuwakaribisha kwetu ili ndoto hiyo itimie.
Mbowe: Sisemi wanaokuja CHADEMA leo wote wana dhambi, hata sisi tulioko CHADEMA leo tuna mapungufu yetu.
Mbowe: Kwahiyo nichukue fursa hii kumkaribisha Edward Lowassa, hawa ndio wenye chama chao sisi wengine wabeba dhamana tu
Mbowe: Kwenye CHADEMA hakuna aliye mkubwa kuliko chama chetu, tukikubaliana tunasonga tunasonga tu.
Mbowe:Yale mabaya mliyokuwa nayo kwenye chama chenu cha zamani tumeyasamehe, tunaomba mtuletee yale mazuri mliokuwa
Mbowe: Hadi siku ya jana Mgombea Mwenza wa CHADEMA alikuwa Waziri Zanzibar lakini ameona ajiuzulu kujiunga na sisi.
Mbowe: Kwa sababu tuna uhakika wa kukamata madaraka ya nchi hii, hiyo sheria tutaibadilisha 'faster'
Mbowe: Naomba nimhakikishie Mh. Duni, yuko kwenye mikono salama na atafanya kazi kikamanda
Mbowe: Ngoja nisome historia ya Edward Lowassa kwa kujidai kidogo, nifute jasho na ninywe maji.
Mbowe: Mh. Lowassa amemuoa mama Regina Lowassa na kujaliwa kupata watoto watano.
Mbowe: Mh. Lowassa ni shabiki mkubwa wa michezo na alikuwa mchezaji mkubwa wa mpira wa kikapu. 'basketball'
Mbowe: Kamati kuu ilifanya utafiti tena ilifanya utafiti kwa vikao vingi mfululizo
Mbowe: Tafiti zetu zilituambia kwamba Mh. Lowassa akipeperusha bendera yetu ndani ya UKAWA, ndoto ya Taifa hili inatimia.
Mbowe: Wote tuliafikiana na kukubaliana kwamba tumpitishe Lowassa, akiwemo katibu Mkuu Dk. Slaa.
Mbowe: Mapendekezo ya Baraza Kuu yamekubali LOWASSA na Haji Duni wapeperushe Bendera ya UKAWA kwenye Urais
Mbowe: Tumependekeza Maalim Seif pekee wa chama cha CUF awe mgombea wa Urais Zanzibar akiwakilisha UKAWA.